728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, February 5, 2016

    Chris Brown:Natengeneza Muziki Mzuri Kwajili ya Mashabiki Wangu.

    Mkali wa muziki wa RnB nchini Marekani, Chris Brown, amesema kwamba anafanya muziki mzuri kwa kuwa huwa anawafikiria zaidi mashabiki wake kabla ya kuandika mashairi.
    550

    Msanii huyo kwa sasa yupo katika mgogoro na Nia Guzman, aliyezaa naye mtoto (Royalty), kwa madai kwamba anamsababisha ugonjwa wa pumu mtoto huyo kutokana na matumizi ya sigara anazovuta Chris Brown.

    “Tangu nimepata mtoto kikubwa ambacho ninakifikiria ni mwanangu na mashabiki wanataka nini katika nyimbo zangu, hali hii imekuwa tofauti na miaka ya nyuma kabla sijapata mtoto.

    “Mashabiki wananifanya nitumie muda mwingi kutengeneza muziki wenye viwango, kikubwa mashabiki wanataka burudani na ndicho ninachokifanya kila siku,” alisema Chris.

    Hata hivyo, msanii huyo amedai kwamba tangu amempata mtoto huyo maisha yake yamebadilika kwa kuwa sasa anaishi maisha ya kiutu uzima.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Chris Brown:Natengeneza Muziki Mzuri Kwajili ya Mashabiki Wangu. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top