728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, February 17, 2016

    MCHEZAJI AMUUA REFARII UWANJANI BAADA YA KULIMWA KADI NYEKUNDU.



    MECHI ya soka nchini Argentina imemalizika katika hali ya kutisha baada ya mchezaji mmoja kumuua refarii uwanjani kwa kumfyatulia risasi tatu na kukimbia. 





    Tukio hilo limetokea katika Wilaya ya Cordoba baada ya refarii huyo, Cesar Flores kumwonyesha mwanasoka huyo kadi nyekundu ya moja kwa moja kutokana na kumpiga mchezaji wa timu pinzani dakika za mwanzoni za mchezo. 

    Polisi imethibitisha tukio hilo na kuongeza kuwa mchezaji huyo aliyempiga Flores risasi kichwani, shingoni na kifuani, pia alimlenga mchezaji mwingine, Walter Zarate ambaye ameripotiwa hali yake kutokuwa mbaya.

    “Yote hayo yametokea wakati wa mechi,” alisema msemaji wa polisi. “Hatujui nini kilitokea kati yake na refarii, lakini mchezaji alikasirika na kwenda kuchukua bunduki yake na kumuua.”

    Mwanasoka huyo ambaye alikuwa na silaha hiyo ndani ya mkoba wake, anatafutwa na polisi baada ya kukimbia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MCHEZAJI AMUUA REFARII UWANJANI BAADA YA KULIMWA KADI NYEKUNDU. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top