728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, February 3, 2016

    Halima Mdee: Hii biashara ya kufanya Rais ashikiki wala hatajwi ‘Ikome’.

    Mbunge wa Kawe jijini Dar es Salaam, Halima James Mdee, jana amezua mjadala bungeni baada ya kuweka wazi kuwa anakerwa na kitendo kinachotajwa na baadhi ya Wabunge kwamba Rais hatajwi wala haguswi na hoja.
    Akichangia Bungeni jana, Mdee alidai wakati Rais Magufuli alipokuwa waziri wa Ujenzi walipanga kukarabati barabara ya kilometa 5004 lakini zikakarabatiwa 2700 pekee.

    Wabunge wa CCM walicharuka wakimtaka Halima, kutotumia wala kumtaja Rais kwa Dhihaka kwa kuwa kanuni za Bunge haziruhusu.
    “Kwa mujibu wa kanuni ya 64 fasili ya kwanza, Mbunge hatotumia kwa dhihaka jina la Rais katika mjadala, Mbunge anayeendelea anatumia jina la Rais kwa Dhihaka naomba aendelee bila kumtaja” Alisikika Mbunge mmoja wa chama cha Mapinduzi.

    Mbunge huyo kijana wa CHADEMA, alijibu hoja hiyo kwa kusema jukumu la Bunge ni kuirekebisha Serikali hivyo yuko sawa kumtaja.

    “Nasema hivi hii biashara ya kufanya rais ni mtu ambae hashikiki wala hatajwi wala haguswi iachwe, kwa sababu jukumu la Bunge ni kuirekebisha na kushauri Serikali” Alisema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Halima Mdee: Hii biashara ya kufanya Rais ashikiki wala hatajwi ‘Ikome’. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top