728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, February 12, 2016

    Yafahamu Makosa 3 Makubwa Yanayokufanya Ushindwe Kutimiza Malengo Yako.

    Ni kitu ambacho kimeshawahi kukutokea ama kuona kwa wengine wakiwa wakitimiza malengo yao na wakati wengine malengo yao yakiwa hayajitimizwa.

    Hii ni hali ambayo huwa inatokea katika maisha yetu mara kwa mara. Na huwa ni kitu cha kuumiza unapoona ndoto zako zinaakwama wakati za wengine zikiwa zinatimia tena bila wasiwasi.
     
    Je, ulishawahi kujiuliza ni kitu gani kinachosababisha ndoto ama malengo ya wengine kutimia na wengine kutotimia. Kwa kawaida wengi huwa ni watu wa kutokujua kuwa, kuna makosa ambayo huwa tunayafanya na kupelekea malengo yetu kutokuweza kutimia. Makosa haya ndiyo huwa kizuizi cha malengo ya wengi kutokutimia.


    Kwa kufanya makosa haya mara kwa mara na bila kujirekebisha ni kitu ambacho kimekuwa kikiua mipango ya wengi. Katika makala hii utajifunza juu ya kuweza kuepuka makosa hayo ambayo yamekuwa yakikwamisha wengi kufikia malengo husikika. Je, unajua ni makosa gani ambayo huwa unayafanya?


    Haya Ndiyo Makosa 3 Makubwa Yanayokufanya Ushindwe Kutimiza Malengo Yako.
      1. Unashindwa kuweka nguvu ya uzingativu pamoja.
    Ili uweze kufanikiwa katika malengo uliyojiwekea ni muhimu sana kwako kuweza kuweka nguvu ya uzingativu kwa pamoja. Bila kufanya hivyo, utakuwa unafanya kosa linalofanya malengo yako yashindwe kutimia. Ni lazima kuweka nguvu za uzingativu katika malengo yako ili kufanikiwa. Nguvu hizi za uzingativu zitafanya kazi kwako ikiwa una tabia ya kupitia malengo yako angalau kila siku bila kuacha.


    Unapofanya hivyo, mawazo yako ya ndani yanakuwa yanakusaidia katika mchakato mzima wa kukamilisha malengo yako. Hilo tunaweza kujifunza zaidi kwenye mwanga wa jua.


    Kwa kawaida mwanga wa jua unapotumika mara nyingi huwa hatuwezi kuona matokeo yake makubwa sana. Lakini mwanga huohuo unapokusanywa kwenye kioo cha lensi huwa una nguvu kubwa sana kiasi cha kutoboa hata chuma.

    Hivi ndivyo nguvu za uzingativu zinavyofanya kazi katika maisha yetu. Zinapotumiwa vizuri huleta athari kubwa. Lakini zinaposhindwa kutumiwa vizuri, hakuna malengo tunayoweza kuyafikia. 


    Kama unataka uone unatimiza malengo yako yote anza kutumia nguvu za uzingativu kwa kuweka uzingativu wa kutosha kwanza kwenye lengo lako moja tu. Acha kuwa na malengo mengi sana kwa wakati mmoja utakosa nguvu hizi na hakuna utakachokamilisha.

    2. Kujiwekea malengo vibaya.
    Kati ya kosa ambalo linafanya baadhi ya watu kushindwa kufikia malengo yao ni kujiwekea malengo vibaya. Kwa kujiwekea malengo yao vibaya, hujikuta ni watu wa kushindwa kutimiza malengo hayo. 


    Watu hawa huweka malengo yao vibaya pengine kwa kujiwekea malengo makubwa sana au ambayo hayana sifa. Malengo kama hayo kwa kawaida huwa hayawezi kufikiwa hata iweje.

    Kwa kuwa na malengo ambayo hayana sifa hilo ndilo kosa ambalo huwa linafanyika. Kama ilivyo kwa sifa za lengo lolote lile ni lazima liwe ni maalum, linapimika, linatekelezeka, linafikika na lina muda pia. Kwa wengi huwa hayana sifa hizo muhimu.


    Ili kufikia malengo uliyojiwekea ni lazima na muhimu lengo lako liwe na sifa kamili, vinginevyo itakuwa ngumu kwako kuweza kufanikisha malengo yako katika maisha kwa sababu utakuwa umejiwekea malengo hayo vibaya.

    3. Kutokujitoa kikmilifu.
    Wengi huwa wanashindwa kutimiza malengo yao kwa sabau siyo hayawezekani kufikika, bali ni kutokana na wao kushindwa kujitoa kikamilifu kuelekea kwenye ndoto na malengo yao. Kwa kushindwa kujitoa mhanga huwa ni ngumu sana kuweza kufikia malengo yao. Kinachotakiwa kwako kufanyika ni nguvu ya kujitoa sana kikamilifu ili kufanikiwa.


    Kumbuka kuwa maisha sio lelemama, hivyo unatakiwa nguvu nyingi na mawazo mengi kuyapeleka kwenye malengo yako mpaka kuweza kufanikiwa. Kinyume cha hapo unakuwa unajipotezea muda mwenyewe maana utajikuta ni mtu ambaye kama mipango na malengo yako haikamiliki hivi. 


    Amua kujipanga na kujitoa kikamilifu kuelekea kwenye malengo yako na ni lazima utafanikiwa.

    Ikiwa wewe ni mhanga wa kuona malengo yako kutokutimia katika maisha yako ni muhimu kujua kuwa unaweza ukawa unafanya makosa sana kama hayo yalivyoelezwa. Hivyo ni muhimu sana kwako kuweza kuyaepuka ili kujihakikishia uwezekano wa kufanikiwa.

    ============================================================
    TANGAZA NASI KWA KUKIDHI VITU VIFUATAVYO;
    1. Biashara / Maduka na Bidhaa / Ofisi 2. Kuuza Nyumba / Kupangisha 3. Kuuza Magari / Pikipiki 4. Kuuza Viwanja / Mashamba 5. Matangazo Mbalimbali 6. Matangazo ya Mikutano / Sherehe 7. Matangazo Shule / Course za Masomo Mbalimbali 8. Hotel / Restaurat

    Tunapokea matangazo  yako sasa Tangaza na TBN_MUSSANKONINGO.BLOGSPOT.COM  kukuza Bishara yako na kuwafikia watu wengi Wasiliana nasi Kwa simu namba 0755933877/0787260182.    Au EMAIL@MUSSABAKARINKONINGO@GMAIL.COM.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Yafahamu Makosa 3 Makubwa Yanayokufanya Ushindwe Kutimiza Malengo Yako. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top