728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, February 4, 2016

    Rapa wa Nigeria adai Wizkid alimuibia wimbo wa ‘Ojuelegba

    Hit maker wa ngoma kadhaa zinazofanya poa nchini Nigeria, Ayodeji Balogun ‘Wizkid’, amedaiwa kuiba wimbo uliofanya vizuri wa  ‘Ojuelegba’.

    Jamaa ambaye ni rapa kutoka mjini Lagos  Ahmedu Augustine ‘Blackface’, amedai kwamba Wizkid amekuwa na tabia ya kuiba nyimbo zake lakini amekuwa kimya kwa muda mrefu ila sasa ameamua kuvunja ukimya wake.

    “Nilikuwa kimya kwa siku nyingi, lakini kwa sasa nimeona bora niweke wazi kwa kuwa kwenye wimbo wangu mpya wa ‘Killa’ midundo yake ni kama wimbo huo wa Wizkid, kitu ambacho sikipendi.

    “Hata hivyo, ukiusikiliza wimbo wangu wa ‘Dancehall’ ambao niliuachia mwaka 2010 unafanana na huu wa Ojuelegba, lakini kikubwa ni kuisikiliza albamu hiyo kisha utagundua ukweli kuhusu hili. Najua hata yeye mwenyewe anajua hilo,” aliandika Blackface kupitia mtandao wa Instagram.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Rapa wa Nigeria adai Wizkid alimuibia wimbo wa ‘Ojuelegba Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top