728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, April 28, 2016

    Afande Sele:wasanii wengine wa bongo fleva wanaimba kuanzisha mabifu.


    Kwenye Exclusive interview na Metro fm 99.4 Msanii mkongwe kwenye muziki wa HipHop Afande Sele,amedai kuwa muziki huo unaonekana kufanya vizuri lakini chipukizi wengi wamekuwa wakiimba mistari ya matusi na si kuelimisha jamii kama muziki unavyotaka.

    Mkongwe huyo kutoka Moro,alidai kuwa kwa muda mrefu amekuwa akiwatazama vijana wanaonekana kuchuana kwenye muziki huo lakini wengi wamekuwa wakiimba kwa ajili ya kumkejeli mwengine.

    Hata hivyo alipoambiwa kumtaja mmoja ya wasanii wa HipHop ambapo anaamini ni wakali,alishindwa kufanya hivyo kwa madai kuwa anaweza kutengeneza bifu kubwa kwa wengine ambao hajawataja,ila anaamini wengi watainuka na kuachana na nyimbo za matusi.

    ”Mara nyingi hula naitazama chi yang na kuona kwamba kuna mambo menage ambayo yanahitajika kuzungumzwa kwa ajili ya kumaliza changamoto zetu,lakini wasanii wengine wanaimba mapenzi,badala ya ujumbe, inasikitisha sana,lakini naamini kwamba muziki wa HipHop ni jibu ingawa hautumika vizuri,” alisema Sele.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Afande Sele:wasanii wengine wa bongo fleva wanaimba kuanzisha mabifu. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top