728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, April 29, 2016

    Hawa ni wachezaji 7 walioweka rekodi kwenye historia ya soka wakiwa na jezi namba 7 mgongoni.

    Chukua hii..!! Suala la wachezaji kuvaa jezi namba flani mgongoni mara nyingi huwa linaongozwa na imani au pengine mapenzi ya mchezaji mwenyewe ,ila hii hapa ni list ya wachezaji saba ambao wamewahi kufanya mambo makubwa kwenye historia ya  soka ulimwenguni,wakiwa wamevaa jezi namba 7 mgongoni.
    Robert Pires alidumu kwenye kikosi cha Arsenal kwa miaka 6 pekee lakini ilitosha  kumpa heshima kwenye klabu hiyo na kuwa miongoni mwa wachezaji wa kukumbukwa kwenye historia ya Arenal.Baada ya mafanikio makubwa kwenye michuano ya kombe la dunia na Euro mwaka 1998 na 2000 akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa, Pires alijiunga na The Gunners na kukiongoza kikosi hicho kutwaa makombe matatu ya FA na mataji mawili ya Premier League.
    Luis Figo anatajwa kama nahodha wa aina yake kuwahi kutokea kwenye timu ya taifa ya Ureno ambaye alikuwa akivaa jezi namba 7 na kupata mafanikio makubwa. Winga huyu  aliekua na uwezo  hali ya juu kipindi cha uchezaji wake, anasifika kwa uwezo wake mkubwa wa kukimbia na mpira huku akiwaacha mabeki ikiwa ni pamoja na  kutengeneza nafasi kwa wachezaji wenzake kufunga mabao.Licha ya kutotwaa  taji lolote akiwa na timu yake ya taifa,Luis Figo lakini anabaki  kuwa miongoni wachezaji bora kuwahi  Ureno na anakumbukwa zaidi na mashabiki wa Inetr Milan na Real Madrid,vilabu alivyowahi kuvitumikia kutokana na uwezo aliounesha kwenye historia ya michezo aliyocheza kwenye timu hizo.
    Kenny Danglish alikuwa ni miongoni mwa wachezaji muhimu ndani ya Liverpool kwenye miaka ya 1970 na1980 na anatajwa kama  wachezaji bora kuwahi kuitumikia Liverpool.Danglish Alichukua namba 7 ambayo ilikuwa inavaliwa na mkongwe mwingine wa Liverpool Kevin Keegan, lakini alifanikiwa kupata mafanikio kuliko alyemtangulia kuvaa jezi hiyo.
    Mashabiki wa soka nchini Uingereza walimpa jina la  ‘Premier League bad boy’,ila ukweli unabaki kuwa Eric Cantona ni miongoni mwa majina yenye heshima kuwahi kuvaa jezi namba 7 kwenye klabu ya Manchester United.
    Licha ya kuchukiwa na baadhi ya mashabiki, Cantona alifanikiwa kuwateka mashabiki wengi wa United kutokana na uwezo alichokuwa anakionesha uwanjani. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alidumu United kwa miaka 5 lakini aliweza kufunga magoli 80 na kushinda mataji kibao ikiwemo ya mataji matatu (treble) mnamo mwaka 1999.


    Garrincha ni jina maarufu kwenye historia ya  soka la Brazil, anasimama kama mchezaji bora kuwahi kutokea amabaye alikuwa akivaa jezi namba 7. Akiwa amekiongoza kikosi cha Brazil kutwaa kombe la dunia mwaka 1972 bila ya Pele. Legend huyo wa Brazil alichaguliwa kwenye kikosi bira  cha  karne ya 20 na timu ya FIFA ya wachezaji bora wa muda wote kwenye kombe la dunia.

    Star huyu anaeichezea klabu  ya Real Madrid anafunga list hii ya wachezaji waliowahi kupata mafanikio wakiwa ndani ya jezi namba 7 huku akiwa bado na muda wa kuendelea kufanya makubwa zaidi.Ronaldo alianza kupata mafanikio kwenye klabu ya Manchester United ambapo alionesha uwezo wa hali ya juu kabla  ya kuhamia Hispania mwaka 2009 na ameendelea rekodi ya kufunga magoli ambayo itawachukua muda mrefu ma-striker wengine  kuivunja rekodi yake.

    Credit : Shafii Dauda.
     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Hawa ni wachezaji 7 walioweka rekodi kwenye historia ya soka wakiwa na jezi namba 7 mgongoni. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top