728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, April 19, 2016

    SERGIO AGUERO KASEMA HAYA KUHUSU KOMBE LA LIGI YA MABINGWA.

    SERGIO AGUERO alipiga mabao matatu wakati Manchester City ikiishinda Chelsea katika Premier League Jumamosi, kisha akaichimba mkwara Real Madrid kuelekea mechi yao ya nusu fainali ya Champions League kwamba taji la michuano hiyo “linawahusu”.

    Akizungumza katika mahojiano na gazeti la Daily Mail baada ya mechi ya Jumamosi, staa huyo raia wa Argentina alisema: "Wakati nilipokuja City, nilisema tunataka kushinda Champions League na sasa tumekaribia. "Natumaini tutapata nafasi. 

    Bado nina miaka michache imebaki hapa na bado tuna uchaguzi, lakini sitakwenda mahali popote, labda tutashinda mwaka huu au labda sivyo. 

    Hata hivyo tunakuwa bora na kukaribia." Mshambuliaji huyo wa kati kisha aliwamwagia sifa Real Madrid kufuatia kutoka nyuma na kushinda dhidi ya Wolfsburg, na akawataka nyota wenzake kuwa na tahadhari na miamba hiyo ya Hispania.

    "Ilikuwa mshangao mkubwa kwetu wakati Wolfsburg waliposhinda mechi ya kwanza, lakini chochote kinaweza kutokea katika Champions League. Nadhani Madrid walijifunza kutoka mechi ya Ujerumani, wana wachezaji wazuri na wanaweza kumfunga mtu yeyote,” alisema
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SERGIO AGUERO KASEMA HAYA KUHUSU KOMBE LA LIGI YA MABINGWA. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top