728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, April 22, 2016

    FARID MUSSA AMEPATA ZALI NCHINI HISPANIA.

    Mchezaji wa Azam FC, Farid Mussa ameitwa Hispania kufanya majaribio. 

    Farid Mussa ni mmoja kati ya wachezaji chipukizi ambao wanafanya vizuri na timu yake ya Azam FC na timu ya taifa.

    Farid amepata nafasi hiyo ya kwenda Hispania kufanya majaribio kwenye timu za Malaga na Las Palmas ambazo zote zinashiriki ligi kuu ya nchi hiyo (La Liga) na atakuwa huko takribani kwa mwezi mmoja na atarejea Tanzania, May.

    Mchezaji huyo bado yupo nchini Tunisia na timu yake ya Azam FC lakini Farid kesho Ijumaa ataondoka kuelekea Hispania akitokea huko huko Tunisia.

    Kila la kheri Farid Mussa, wewe ni mmoja wa wachezaji ambao tunawategemea kuja kuipandisha timu yetu ya taifa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: FARID MUSSA AMEPATA ZALI NCHINI HISPANIA. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top