728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, April 14, 2016

    MWAKYEMBE AGOMA KUPOKEA MALALAMIKO YA WANANCHI.

     
    Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Harrison Mwakyembe (pichani) amewataka wananchi kutomwandikia barua za malalamiko yao, badala yake watumie kamati za maadili za kimahakama zilizopo kila Wilaya nchini ili kupata haki zao.

    Mwakyembe ametoa kauli hiyo hii leo Jijini Mwanza, anakofanya ziara ya kikazi ili kujionea utendaji kazi wa idara mbalimbali zikiwemo za mahakama.

    "Tumeunda kamati za maadili za mahakama hivyo pelekeni barua za malalamiko kwenye hizo kamati ambazo mwenyekiti wake ni Mkuu wa Wilaya". Amesema Mwakyembe huku akimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Baraka Konisaga kwa kuunda kamati hiyo ambayo ndani yake pia yumo Katibu tawala Wilaya, Jaji Mfawidhi na hakimu wa Wilaya.

    Amesema kwa siku amekuwa akipokea barua za malalamiko zaidi ya 40 kutoka kwa wananchi nyingi zikitoka Mkoani Mwanza, hivyo wananchi watumie kamati za maadili katika wilaya zao ili kutatua malalamiko yao ikizingatiwa kwamba kamati hizo zinafanya kazi inavyostahili.

    Aidha Dkt.Mwakyembe amesikitishwa na vitendo vya Mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi Mkoani Mwanza, hivyo amepiga marufuku mauaji hayo kujirudia kwani yameiweka Tanzania katika sura ya aibu kimataifa. Amesema Mwanza inaongoza katika mauaji hayo ikifuatiwa na Kagera na Geita.

    Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MWAKYEMBE AGOMA KUPOKEA MALALAMIKO YA WANANCHI. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top