728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, April 28, 2016

    Kwa mara ya kwanza Fainali ya UEFA itakuwa na tukio hili kubwaa…


    Mechi za Nusu Fainali ya Uefa bado  zinaendelea huku mechi iliyochezwa juzi Manchester City walitoka sare na Real Madrid, huku Timu ya soka ya Atletico Madrid ikiichapa Goli Moja bila majibu timu ya Bayern Munich.

    Fainali ya UEFA itachezwa huko Milan Italy na tayari imethibitishwa msanii mashuhuri Alicia Keys ndio atafungua sherehe za msimu huu wa kombe la UEFA katika dimba la Stadio Giuseppe Meazza nchini Milan.
    Kwa mara ya kwanza katika historia ya mpira wa miguu kutakuwa na burudani ya muziki kabla ya fainali kuanza rasmi May 28. 2016 Fainali hiyo ya UEFA inatazamiwa kutangazwa ndani ya nchi 220 na kutazamwa na watazamaji Milioni 180  katika nchi zote Duniani. 
    Alicia key
    Hatua ya nusu fainali ya kwanza imekamilika jana kwa kushuhudia Manchester city vs Real madrid wakienda sare 0-0 huku Atletico madrid wakishinda 1-0 dhidi ya vigogo wa Bundesliga Beryen munich na kinachosubiriwa na mashabiki ni kuona michezo ya marudiano ambayo itaaamua nani atakwenda kucheza fainali katika uwanja wa Stadio Giuseppe Meazza mjini Milan nchini Italy.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Kwa mara ya kwanza Fainali ya UEFA itakuwa na tukio hili kubwaa… Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top