728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, April 29, 2016

    Nape Nauye Kayasema haya kwa Madansa wa kibongo... Nao kutambulika Ulimwenguni.

    Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye anatarajia kuzindua siku ya madansa duniani itakayoadhimishwa kwenye viwanja vya TCC Club Chang’ombe, Dar es Salaam leo.

    Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Tanzania Disc Association (TMDA), Asanterabbi Mtaki, inaeleza kwamba kwa mara ya kwanza madansa nchini wataungana na madansa wa mataifa mengine duniani kuadhimisha siku hiyo inayoadhimishwa kila Aprili 29 ya kila mwaka.

    “Lengo la maadhimisho hayo hapa nchini ni kuhamasisha madansa kushiriki, kujitolea kufanya shughuli za kijamii kivitendo na kuongeza uelewa ili wajitambue kuwa ni sehemu ya ajira ya kujipatia kipato,” alieleza Mtaki.

    Alisema baadhi ya madansa waliojitokeza kushiriki katika maadhimisho hayo ni Bombes group, Wakali Dancer, Athuman digadiga bingwa wa break-dance na funky Taifa pamoja na madj mbalimbali akiwemo Dj Seckklito, Dj john Peter Pantalakis, Dj disko na Dj Mafuvu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Nape Nauye Kayasema haya kwa Madansa wa kibongo... Nao kutambulika Ulimwenguni. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top