728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, April 18, 2016

    MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU AMFUTA MACHOZI MILLEN MAGESE MAPAMBANO DHIDI YA ENDOMETRIOSIS.

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mama Samia Suluhu amemfuta machozi Mwanadada,Happiness Millen Magese ambaye ni shujaa wa kipekee kutoka Afrika dhidi ya mapambano ya ugonjwa wa Endometriosis.

    Mama Samia amechukua hatua hiyo jioni ya 15 Aprili 2016 wakati wa hafla maalum ya kumkabidhi tuzo.

    Katika kilio chake hicho Millen, kimemfanya Mama Samia kumfuta machozi na kumpa kitambaa, mwanamitindo huyo huku akimweleza kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana naye kwani tatizo hilo si la Millen pekee bali ni kwa wanawake wengi hapa Tanzania.

    Mama Samia alimwambia kuwa, tatizo alilonalo la kuziba kwa mirija ya uzazi lipata ufumbuzi na kutaka asilie kwani Serikali inania njema kwa watu wake hivyo wataendeleza juhudi Zaidi huku akifungua milango na mwanadada huyo.

    Suluhu alisema kuwa hata yeye tatizo kama hilo lipo katika familia yake, lakini ana amini kwa ushirikiano wa mwanamitindo huyo tatizo hilo linapewa uzito. Alisema kuwa ni kitu kilichokuwa kikimuumiza sana kichwa, ana amini kupitia Millen hata binti yake atapata nafuu.

    "Nimefurahi kukutana nawe na Serikali haitakuangusha tutakuunga mkono katika kuhakikisha gonjwa hili linapata ufumbuzi na kutoa elimu kwa kila mtanzania kulitambua"alisema.

    Akizungumza kwa upande wake Magese alisema amekuwa akifanya semina mbalimbali kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa Hospitali ya Taifa, Muhimbili, kuwaelimisha wanawake kuhusu endometriosis.

    "Ninaamini -Nikiokoa hata nafsi moja kuna wakati ambao inatosha kwani nafsi hiyo yaweza kuokoa walio wengi zaidi,shabaha yake ni kuona wanawake wenye ugonjwa huo wanapata tiba mapema ili waweze kubaki na uwezo wao wa kushika mimba na kuzaa kwa njia ya kawaida" alisema Magese.

    "Mimi nilichelewa na nimejikuta nikipoteza uwezo wa kushika mimba, kwa hiyo siwezi tena kupata mtoto kwa njia ya kawaida, Kibaiolojia.

    "Nimeshafanyiwa oparesheni mara 13 kati ya Afrika Kusini na Marekani. Na sasa mirija yangu yote ya uzazi imeziba, vilevile upande mmoja wa ovari haufanyi kazi".

    "Naahidi kupambana na ugonjwa huu mpaka mwisho. Pamoja na jitihada zote, lengo langu la juu ni kuhakikisha napata uwezo wa kujenga hospitali kubwa kupitia taasisi yangu ya Millen Magese (Millen Magese Foundation) ambayo itajishughulisha zaidi na utoaji wa tiba ya endometriosis kwa wanawake. Namuomba sana Mungu anisaidie."
    Picha zaidi hapa chini..........















    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU AMFUTA MACHOZI MILLEN MAGESE MAPAMBANO DHIDI YA ENDOMETRIOSIS. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top