728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, April 22, 2016

    Msanii huyu mchanga aachwa na mpenzi wake baada ya kudai kuwa ana ndoto ya kumuoa Vanessa Mdee.

    Vanessa Mdee amempoza Bright, msanii mchanga aliyedai kuwa ana ndoto ya kuja kumuoa.

    “Nataka kumuoa, Vee Money ni mwanamke mzuri kwanza, ni mwanamke mwenye mvuto ambao mwanaume yeyote aliye kamili lazima avutiwe naye.” Bright alifunguka hivi karibuni alipokuwa akifanya mahojiano na Planet Bongo ya East Africa Radi huku akijitapa kuwa hajali kama Vee Money yupo na Jux kwa sasa.

    Kauli hiyo imemtokea puani msanii huyo, Mpenzi wake amemuacha na kumtaka akamuoe Vanessa.
    Planet Bongo imepata audio ya maongezi ya wawili hao ambapo binti huyo amesikika akisema kama hataki tena kuwa na mahusiano na msanii huyo  na kumtaka akamuoe Vanessa aliyemtaja kwenye media.

    Bright ameachia wimbo wake wa ‘Nitunzie’ aliomshirikisha Baraka Da Prince.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Msanii huyu mchanga aachwa na mpenzi wake baada ya kudai kuwa ana ndoto ya kumuoa Vanessa Mdee. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top