728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, April 24, 2016

    Ni Haki yako kuijua Meli Kongwe Nchini.

    Limbo lya Mfipa ” ni jina la kabila la Warungu. Kwa tafsiri ya moja kwa moja kwa lugha ya Kiswahili ni Ziwa Tanganyika.

    Warungu Ziwa Tanganyika wanaliita “Liemba lya Mfipa”. Warungu wanapatikana katika vijiji vilivyopo katika mwambao mwa Ziwa Tanganyika kata ya Kasanga wilayani Kalambo na ni miongoni mwa makabila katika mkoa wa Rukwa. Kabila kubwa mkoani humo ni Wafipa.
     
    Jina hilo la Mv Liemba ni la meli ya kivita ya Ujerumani ambayo ilinunuliwa baada ya kutekwa vitani na Uingereza. Ilinunuliwa kwa Sh 60,000 tu baada ya nchi ya Ujerumani kushindwa katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.

    Meli hiyo imetajwa kwenye kitabu cha kumbukumbu za dunia Guiness World Book of Records kama ndio meli kongwe zaidi ulimwenguni ambayo bado inaendelea kutoa huduma ya kubeba abiria na mizigo. Kwa sasa ina umri wa zaidi ya miaka 113 (1913 -2016) na bado inaendelea kutoa huduma.

    Mv Liemba inaendelea kutoka huduma katika Ziwa Tanganyika na ndio meli kubwa kuliko zote inayohudumu kubeba abiria ziwani humo. Ziwa Tanganyika lina kina na maji chenye umbali wa kilomita moja na nusu .

    Inafanya safari zake kutoka bandari ya Kigoma (Tanzania), Kalemie na Moba katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mpaka bandari ya Mpulungu nchini Zambia kupitia bandari ndogo ya Kasanga wilayani Kalambo katika mkoa wa Rukwa .
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Ni Haki yako kuijua Meli Kongwe Nchini. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top