728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, April 28, 2016

    Facebook kula shavu nono kwenye faida kupitia Matangazo.

    Facebook imeripoti ongezeko la faida kwa asilimia 195 katika robo ya kwanza ya mwaka huku kampuni hiyo ikiendelea kupata mapato ya matangazo mapya.

    IIiripoti mapato ya dola bilioni 1.5 katika kipindi cha kati ya mwezi Januari na Machi ikilinganishwa na mapato ya dola milioni 512 mwaka uliopita.

    Mbali na kuwapatia wenye matangazo huduma mpya kama vile video, Facebook iliimarisha mauzo yake kutokana na huduma zilizopo.

    Facebook pia imependekeza mpango mpya wa hisa ambao utampatia fursa mwanzilishi wake Mark Zuckerberg kuuza hisa zake bila kupoteza udhibiti wa kampuni hiyo.

    Kampuni hiyo imesema kwamba hatua hiyo itampa moyo bwana Zuckerberg kusalia katika uongozi wa facebook.

    Thamani ya hisa za facebook ilipanda hadi asilimia 9 baada ya kufanya biashara.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Facebook kula shavu nono kwenye faida kupitia Matangazo. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top