728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, April 30, 2016

    Hii Ndiyo Mipango ya Nay wa Mitego kuachia wimbo mpya ambao ni mbadala wa ‘shika adabu yako’ uliofungiwa na (BASATA).

    Rapa elibariki Emmanuel ‘Nay Wa Mitego’ kwenye Exclusive na 99.4 Radio Metro fm kupitia kipindi cha Friday Club Mix amesema kuwa mwanzoni mwa mwezi ujao ataachia wimbo mpya ambao ni mbadala wa ‘shika adabu yako’ uliofungiwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).

    Msanii huyo alisema kuwa anatarajia wimbo huo mpya ambao bado hajaupa jina utapendwa na mashabiki wa miziki wa kizazi kpya kutokana na mashairi yake kuyapangilia vyema.

    “Mei 9 mwaka huu nitaachia wimbo na video ya wimbo wangu mpya ambao ninaamini kuwa ni mkali kuliko ‘Shika Adabu Yako,” alisema Nay wa Mitego na kuongeza:

    “Ninajua wimbo wa Shika Adabu Yako bado unafanya vizuri,lakini nimeamua kuandaa mbadala wake baada ya kufungiwa ingawa tayari mashabiki walishaupata.”

    Rapa huyo alisema kuwa Juni atafyatua video ya wimbo mwingine ikiwa ni mikakati yake ya kuandaa nyimbo mfululizo ili kukidhi kio ya mashabiki wake.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Hii Ndiyo Mipango ya Nay wa Mitego kuachia wimbo mpya ambao ni mbadala wa ‘shika adabu yako’ uliofungiwa na (BASATA). Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top