728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, April 14, 2016

    PRIYANKA CHOPRA AALIKWA IKULU YA MAREKANI KUPATA MLO NA RAIS OBAMA.


    STAA wa kike wa Bollywood, Priyanka Chopra, amealikwa kula chakula cha jioni katika Ikulu ya Marekani pamoja na Rais Barack Obama na mkewe Michelle mwishoni mwa mwezi huu, lakini amesema hana uhakika kama atahudhuria hafla hiyo kwa kuwa hivi sasa yuko ‘bize’ na miradi yake.

    Hafla hiyo huandaliwa kila mwaka na Chama cha Waandishi wa Habari za Ikulu ya Marekani (WHCA), ambacho wanachama wake hujumuisha waandishi, maprodyuza, waendeshaji kamera, ikiwa na lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya masomo ya uandishi wa habari. 

    Staa huyo wa filamu ya “Mary Kom” aliyetambulishwa kimataifa na tamthiliya ya “Quantico” inayorushwa na Televisheni ya ABC ya Marekani akitumia jina la Alex Parrish, ameelezea shaka yake juu ya kutohudhuria hafla hiyo kutokana na kubanwa na ratiba ya utayarishaji wa tamthiliya hiyo sambamba na filamu yake ya kwanza akiwa Hollywood, “Baywatch”. “Hivi sasa niko ‘busy’ sana na “Quantico” na “Baywatch”. 

    Hiyo ndiyo maana sina uhakika kama nitakula pamoja na Obama. Si kwamba sitaki, lakini sina uhakika,” alisema Priyanka baada ya kukabidhiwa Tuzo ya Heshima ya Raia na Rais wa India, Pranab Mukherjee Jumanne. “Kama nitapata nafasi ya kuwapo, nitamuuliza Obama, ‘utafanya nini ukiwa kipindi chako cha mwisho katika Ikulu ya Marekani’,” alitania staa huyo wa filamu ya “Bajirao Mastani” ambaye pia anafanya kazi zake za filamu nchini Marekani.

    Priyanka aliyeibuka mshindi wa shindano la Miss World mwaka 2000, amealikwa katika chakula hicho cha jioni sambamba na baadhi ya mastaa wenye majina makubwa Hollywood kama Bradley Cooper, Lucy Liu, Jane Fonda na Gladys Knight.
     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: PRIYANKA CHOPRA AALIKWA IKULU YA MAREKANI KUPATA MLO NA RAIS OBAMA. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top