Shirikisho la Soka Afrika limeongeza idadi ya timu za kuingia hatua
ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho
kutoka nane za makundi mawili hadi 16 za makundi manne kuanzia mwaka
ujao.
Hayo yamesemwa na Rais wa CAF, Issa Hayatou katika hotuba ya ufunguzi
wa Mkutano Mkuu wa shirikisho hilo jana Mexico City nchini Mexico.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na Rais wa FIFA, Gianni Infantino,
aliyeongozana na magwiji wa soka, Samuel Eto’o Fils, Luis Figo, Zvonimir
Boban, Hayatou alisema mfumo huo utaanza mwakani.
Mfumo wa sasa wa makundi mawili ya timu nne kila moja, washindi
wawili wa kila kundi hutinga Nusu Fainali na baadaye timu zinazoshinda
kukutana fainali.
Wazi katika mfumo mpya wa makundi manne, kila kundi litatoa timu moja ya kwenda Nusu Fainali.
0 comments:
Post a Comment