Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps ametaja
kikosi cha wachezaji 23, ambacho kitashiriki fainali za mataifa ya
barani Ulaya (Euro 2016) zitakazofanyika kuanzia mwezi ujao.
Deschamps amemuita mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud, huku
akimuweka katika kikosi cha kusubiri mshambuliaji Hatem Ben Arfa ambaye
ameonekana kuwa na msimu mzuri akiwa na klabu ya Nice inayoshiriki ligi
ya nchini Ufaransa.
Wengine waliotajwa kwenye kikosi hicho ambacho kitakuwa na jukumu la
kuwa mwenyeji wa fainali za Euro 2016, ni kiungo wa klabu bingwa nchini
England, Leicester City, N’Golo Kante pamoja na kiungo mshambuliaji wa
West Ham Dimitri Payet.
Hata hivyo kocha Deschamps, anatarajiwa kutaja kikosi cha mwisho
atakachoingia nacho mashindanoni Mei 31, ambapo itakua tarehe ya mwisho
ya kuwasilisha majina ya wachezaji wa timu shiriki mbele ya shirikisho
la soka barani Ulaya UEFA.
Kikosi kamili kilichotajwa na kocha Deschamps upande wa makipa
yupo Hugo Lloris (Tottenham Hotspur), Steve Mandanda (Olympique
Marseille) na Benoit Costil (Stade Rennes).
Mabeki: Raphael Varane (Real Madrid), Laurent
Koscielny (Arsenal), Eliaquim Mangala (Manchester City),
Jeremy Mathieu (Barcelona), Patrice Evra (Juventus), Bacary
Sagna (Manchester City), Lucas Digne(AS Roma) na Christophe
Jallet (Olympique Lyon)
Viungo: Paul Pogba (Juventus), Blaise
Matuidi (Paris St Germain), Lassana Diarra (Olympique Marseille), N’Golo
Kante (Leicester City), Yohan Cabaye (Crystal Palace) na Moussa
Sissoko (Newcastle United)
Washambuliaji: Antoine Griezmann (Atletico Madrid),
Dimitri Payet (West Ham United), Anthony Martial(Manchester
United), Kingsley Coman (Bayern Munich), Olivier Giroud (Arsenal) na
Andre-Pierre Gignac(UANL Tigres)
Kikosi cha akiba: Alphonse Areola (Villarreal),
Hatem Ben Arfa (Nice), Kevin Gameiro (Sevilla), Alexandre
Lacazette (Olympique Lyon), Adrien Rabiot (Paris St Germain, Morgan
Schneiderlin (Manchester United), Djibril Sidibe (Lille) na Samuel
Umtiti (Olympique Lyon).
0 comments:
Post a Comment