Jaji nchini Marekani ameamuru mchekeshaji, Bill Cosby, kusimama mahakamani dhidi ya kesi kwa madai ya unyanyasaji wa kijinsia.
Cosby anatuhumiwa kwa makosa ya kumdhalilisha wanawake katika makazi
yake mnamo mwaka 2004 baada ya kumlewesha kwa kitu kinachodaiwa dawa za
kulevya.
Mchekeshaji huyo,ambaye awali kabla ya masahibu haya alikuwa ni mmoja
miongoni mwa wachekeshaji maarufu wa runinga nchini Marekani, tayari
amekwisha kumbana na misukosuko ya kukabiliwa na wimbi la madai
unyanyasaji wa kijinsia.
Wanawake waliowengi, ambao alikuwa na mahusiano nao miaka ya 1960 wao
hawawezi tena kufungua mashtaka ya jinai.Kufuatia hali hiyo Cosby
amekana madai yote yanayomkabili.
Mwezi uliopita mahakama ya rufaa ilitupilia mbali madai yanayomkabili
Cosby na kusema kwamba alikuwa kinga ya mashtaka kutoka upande wa
mashitaka na aliyekuwa Mwanasheria wa wilaya muongo mmoja uliopita.
0 comments:
Post a Comment