Friday, May 20, 2016
Mamlaka ya
Mawasiliano nchini (TCRA), imeendelea kuwakumbusha watumiaji wa simu za mkononi
kuhakiki simu zao kabla mamlaka hiyo haijazima simu bandia ifikapo Juni 16
mwaka huu.
Akizungumza
kwenye semina ya wadau wa mawasiliano wakiwemo wauzaji wa simu, Mafundi wa
simu, wanahabari pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama, Meneja Mawasiliano wa
TCRA, Innocent Mungi, amesema takwimu za mpaka mwezi Machi mwaka huu,
zinaonesha kuwa asilimia tatu ya simu zinazotumika nchini ni bandia.
Amesema asilimia 13
ya simu zote nchini ni zile zilizonakilishwa na kwamba idadi ya simu hizo
zilizonakilishwa imepungua kutoka asilimia 30 kutokana na elimu inayoendelea
kutolewa na TCRA.
Ametanabaisha
kwamba simu bandia zimekuwa zikiingizwa nchini na baadhi ya wafanyabiashara
wasio waaminifu ambao wamekuwa wakitoa punguzo kubwa la bei kwa wateja
wanaonunua simu hizo na hivyo kuwahamasisha watu wengi kununua simu bandia.
Uchunguzi
uliofanywa na TCRA umebaini kuwa wastani wa bei ya simu halali kwa Tanzania ni
kati ya shilingi elfu 20 hadi elfu 60, bei ambayo wananchi wengi wanao uwezo wa
kununua simu halali hivyo waachane na matumizi ya simu bandia kwani zina
madhara makubwa.
Kujua
ikiwa simu yako ni halali, unapaswa kutuma nambari za simu yako (IMEI Namba)
kwenda 15090 ambapo utapokea ujumbe mfupi wa maneno ukikujulisha ikiwa simu
yako ni bandia (fake) ama halali (Orginal) hii ikiwa ni bure kwa watumiaji wa
mitandao yote.
Related Posts
Donny Roberty Mshindi Miss Mwanza 2016 Tazama Picha hapa chini.
Usiku wa jana Ijumaa Agost 19,2016 kuamkia leo Jumamosi Agost 20,20...
MAONESHO YA BIASHARA ROCK CITY MALL MWANZA.
Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda n...
TFF Yatoa Angalizo Kwenye Msimu Mpya Wa VPL 16-17.
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/17 inatarajiwa kuan...
Sumatra Imesema hakuna usafiri utakaositishwa.
MAMLAKA ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imewatoa hofu ...
Hesabu inaendelea Ibra aweka mbili Nyumbani (VIDEO).
Endeleeni kuhesabu, ndiyo lugha rahisi unayoweza kuitumia baada...
Mambo 8 Yatakayokusaidia Kufikia Malengo Yako.
Kila wakati wengi wetu katika maisha, ni watu wa kujiwekea malengo....
Mkurugenzi Atishia Kuitisha Daftari la Mahudhurio saa tisa Usiku sababu Je?
Normal 0 false false false EN-U...
Gwajima atiwa Nguvuni na Polisi Dar, Imekuaje?
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limemkamata ...
Baada ya Cameroon huyu ndio kuwa Waziri mkuu wa Uingereza.
Katika saa au siku kadhaa zijazo, Waziri wa maswala ya nda...
ULIPITWA; MATOKEO YA ENGLAND VS RUSSIA YAKO HAPA.
June 11 2016 michuano ya Euro 2016 inayofanyika Ufaransa imeen...
- Blogger Comments
- Facebook Comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment