Halmashauri ya Jiji la Mwanza imejipanga kujenga masoko na kuboresha miundombinu yake katika maeneo yaliyopangwa kwa ajili ya machinga kufanyia biashara zao.
Kauli hiyo
imetolewa jana na Mkurugenzi wa Jiji hilo,Adam Mgoyi katika kikao cha
baraza la madiwani, kilichofanyika katika halmashauri hiyo.
Hii ni baada ya
Diwani wa Kata ya Butimba, John Pambalu, kutaka kufahamu halmashauri
hiyo ina mkakati gani wa kuboresha soko la machinga lililopo Mlango
mmoja, ili liweze kuwanufaisha wafanyabiashara wengi na kukuza pato
katika halmashauri hiyo.
Mgoyi alisema,
sheria ndogo za jiji haziruhusu machinga kuzagaa katikati ya mji, hivyo
kupitia kikao cha baraza lililopita, waliamua wafanyabiashara hao,
kwenda katika maeneo waliopangiwa endapo halmashauri hiyo itaweka
mazingira mazuri ya kufanyia biashara na kuboresha miundo mbinu.
Pia alisema,
watashirikisha madiwani wa kata zote zilizopo ndani ya halmashauri hiyo,
wakati wa kujenga na kuboresha miundo mbinu ya masoko, ili kutatua
changamoto za machinga ikiwemo kuzagaa ovyo mitaani.
Aidha alisema
halmashauri inamkakati wa muda mrefu wa kuboresha soko la Mlango mmoja
kwa kujenga ghorofa moja, ambayo itaweza kuwanufaisha wafanyabiashara
wengi na hivyo kuongeza mapato ya halmashauri.
Judith Ferdinand, Mwanza.
0 comments:
Post a Comment