Mrembo Rihanna amejitolea kufadhili elimu ya wanafunzi kupitia wakfu wake hatua hiyo inaamanisha kwamba watu kutoka jamii zisizojiweza watapata msaada wa kulipa ada ya shule.
Wakfu huo wa Clara Lionel umekuwa ukifanya kazi tangu 2012 ambapo
hutoa ruzuku kwa shule huko Barbados mbali na kuwasaidia wagonjwa wa
saratani.
Bibiye Rihana alifariki kutokana na ugonjwa wa saratani mwaka huo huo
na hivyobasi kumfanya yeye kuanza kusaidia sekta ya matibabu.
Kwa sasa shirika hilo limepanuka na kutoa ufadhili wa elimu hadi
kufikia dola 50,000 kwa wanafunzi waliopo
Barbados,Brazil,Cuba,Haiti,Guyana,Jamaica na Marekani.
”Sidhani kwamba ni haki kwa watoto kubeba mzigo wa kifedha katika miaka walio nayo”,alisema Rihanna.
0 comments:
Post a Comment