Nchini Rwanda, mipira ya kondomu imeanza kutolewa bure katika baadhi ya mitaa jijini Kigali ambayo inaaminika kuwa imekithiri kwa ukahaba na kuwa na idadi kubwa ya walioambukizwa virusi vya Ukimwi.
Vibanda vidogo vimewekwa katika mitaa hiyo kwa ajili ya huduma hiyo inayopatikana kwa saa 24.
Wizara
ya afya ya Rwanda inasema asilimia 3 wa wananchi wanaishi na virusi vya
Ukimwi na kwamba zoezi hilo litasaidia kupunguza kasi ya uambukizaji.
“Tulishuhudia
watu wanaoacha kutumia mipira ya kondomu kwa sababu wameikosa, tukaamua
kuleta hivi vibanda katika mitaa hii minne ya jiji la Kigali yenye
kiwango cha juu cha maambukizi ya virusi vya Ukimwi,” anasema Dkt Sabin
Nsanzimana, mmoja wa wanaohusika katika mpango huo.
Wizara ya afya ya Rwanda inasema imekuja na mbinu hii mpya ya
kusambaza kondomu kwa bure baada ya kuona kwamba baadhi ya watu
hushindwa kumudu bei ya kawaidia ya kondomu na wengine kuona haya
kununua kondomu hadharani.
Bei ya kondomu kwenye maduka imekuwa kati ya Franka 300 na 500 za Rwanda ambazo ni karibu nusu dola ya Kimarekani.
Kupitia mpango huu Rwanda inalenga kusambaza mipira ya kondomu milioni moja ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Mwandishi
wa BBC aliyepo Rwanda Yves Bucyana anasema miaka 5 iliyopita Rwanda
ilijaribu mpango ambao haukufanikiwa wa kusambaza kondomu kwa kutumia
mashine zilizowekwa katika sehemu za burudani.
Ili kupata kondomu ilibidi kutumbukiza vichele ndani ya mashine hizo ambazo katika sehemu nyingi sasa zimekwishaharibika.
0 comments:
Post a Comment