Uongozi wa Manchester United, umemtaka meneja wa sasa Louis van Gaal
kuendelea kusalia klabuni hapo kama mkurugenzi wa soka, ili kupisha ujio
wa Jose Mourinho katika benchi la ufundi.
Van Gaal, ametakiwa kubadili upepo wa uongozi wake klabuni hapo, kwa
kupewa jukumu zima la kusimamia masuala yote ya soka sambamba na kubaki
kama mshauri wa benchi la ufundi, ambalo huenda likaendeshwa na Mourinho
kama mipango itakwenda vyema.
Anayefanya kazi ya ushauri huo kwa Van Gaal, ni mtendaji mkuu wa Man
Utd, Ed Woodward na anaamini hakuna jambo lolote litakalo badilika kama
watafikia makubaliano na meneja huyo kutoka nchini Uholanzi.
Hata hivyo Van Gaal ambaye tayari ameshatumikia miaka miaka miwili
katika mkataba wake wenye muda wa miaka mitatu, bado hajatoa jibu kamili
la kukubaliana na mpango huo mpya.
Lakini pamoja na kuwepo kwa kigugumizi cha kutolewa kwa majibu,
tayari Woodward ameshawahakikishia wajumbe wa bodi ya Man Utd, juu ya
jambo hilo kuwezekana kwa asilkimia zote, ili kupisha utawala mpya wa
benchi la ufundi chini ya Mourinho.
Meneja huyo kutoka nchini Ureno, ambaye ameshawahi kuzinoa klabu za
FC Porto, Chelsea, Inter Milan pamoja na Real Madrid, ameshakataa ofa
kadhaa zilizolengwa kwake, kwa kuamini ana kila sababu ya kutajwa kama
mkuu wa benchi la ufundi huko Old Trafford.
0 comments:
Post a Comment