Friday, May 27, 2016
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la PAULO PASCHAL
mwenye umri wa miaka 40 Mkazi wa magu Mkoani Mwanza amenusurika kifo baada ya
kujirusha kutoka katikati ya mnara wa simu uliopo barabara ya makongoro-Airpot jijini
Mwanza.
Akijibu swali kwanini amepanda juu
ya mnara Huo na kutaka kujiua akiwa katika hospitali ya sekour Toure bwana
Paulo paschal amesema alilazimika kufanya hivyo kutokana na Jeshi la polisi
kushindwa kusikiliza kesi zake kama mtuhumiwa sambamba na hilo amesema usiku wa
kuamkia leo baadhi ya watu waliokuwa
wakimfukuza kwa lengo la kutaka kumuuwa hivyo katika hatua ya kujinusuru
alilazimika kuingia katika mnara huo.
Mashuhuda wa tukio wamesema huenda
kijana huyo amefikia maamuzi hayo kutokana na ugumu wa maisha ambao amekuwa
akiulalamikia huku wengine wakisema ni kutokana na kuathiriwa na matumizi ya
dawa za kulevya ambayo amekuwa akiyatumia.
Kwa upande wake HERIETS MADAKTA
Muuguzi wa zamu ambaye amempokea bwana Paulo katika hospitali ya mkoa Sekour
Toure amesema bwana PAULO hana mvunjiko wowote katika mwili tofauti na michubuko katika mwili wa kijana
huyo.
Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa
jeshi la uokoaji na zima moto mkoani Mwanza, Kaimu kamanda wa jeshi la Hilo
Mussa Kaboni, ametoa rai kwa makampuni yenye minara ya simu kuimarisha ulinzi
katika minara hiyo ili kuondoa hatari inayoweza kujitokeza kutoka kwa raia
wasio wema.
Aidha Zoezi la uokoaji lilichukua zaidi ya masaa sita likianza
saa Tatu asubuhi mpaka saa sita mchana.
Picha zaidi Hapa chini.
Picha na Binagamediablog.
Related Posts
Donny Roberty Mshindi Miss Mwanza 2016 Tazama Picha hapa chini.
Usiku wa jana Ijumaa Agost 19,2016 kuamkia leo Jumamosi Agost 20,20...
MAONESHO YA BIASHARA ROCK CITY MALL MWANZA.
Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda n...
TFF Yatoa Angalizo Kwenye Msimu Mpya Wa VPL 16-17.
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/17 inatarajiwa kuan...
Sumatra Imesema hakuna usafiri utakaositishwa.
MAMLAKA ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imewatoa hofu ...
Hesabu inaendelea Ibra aweka mbili Nyumbani (VIDEO).
Endeleeni kuhesabu, ndiyo lugha rahisi unayoweza kuitumia baada...
Mambo 8 Yatakayokusaidia Kufikia Malengo Yako.
Kila wakati wengi wetu katika maisha, ni watu wa kujiwekea malengo....
Mkurugenzi Atishia Kuitisha Daftari la Mahudhurio saa tisa Usiku sababu Je?
Normal 0 false false false EN-U...
Gwajima atiwa Nguvuni na Polisi Dar, Imekuaje?
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limemkamata ...
Baada ya Cameroon huyu ndio kuwa Waziri mkuu wa Uingereza.
Katika saa au siku kadhaa zijazo, Waziri wa maswala ya nda...
ULIPITWA; MATOKEO YA ENGLAND VS RUSSIA YAKO HAPA.
June 11 2016 michuano ya Euro 2016 inayofanyika Ufaransa imeen...
- Blogger Comments
- Facebook Comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment