Kuna mambo mengi usiyoyajua kuhusu ikulu ya marekani ambayo pengine kwa msomaji anaweza kushangazwa akiyajua.Hivyo katika kusherehekea Sikukuu ya Rais baadhi ya watu waliweza kutoa mambo 11 kuhusu ikulu
ya Marekani ambayo ina jumla ya vyumba 132 na imejengwa katika eneo la
ukubwa wa mita za mraba 17,000. Mambo hayo ni haya yafuatayo:
Awali ilijulikana tu kama jengo la West Wing ni ofisi za watendaji. West Wing ilijengwa na Rais Teddy Roosevelt akiwa na lengo la kutenganisha makazi na sehemu za ofisi. Hata hivyo alipoingia madarakani Rais Taft
akaamua kuunganisha jengo la ofisi la West Wing na majengo ya makazi
akisema anataka kuhusika zaidi na shughuli zzote za White House.
Ndani ya ikulu ya Marekani kuna nyumba pacha ambapo inaelezwa kuwa James Hoban ni
mbunifu na raia wa Ireland alichora kwa mfano wa jengo la Leinster la
jijini Dublin huko Ireland. Awali jengo la Leinster lilikuwa makazi ya
kiongozi wa Leinster na kwa sasa ni jengo la bunge la Ireland. Kwa
maneno mengine White House ya Marekani inashabihiana na jengo la bunge
la Ireland.
Katika ikulu ya marekani hakuna kitu kama chakula cha bure, hata kwa Familia ya rais wa nchi hiyo.Mwishoni mwa kila mwezi, Rais anapata bili yake binafsi ya kulipia chakula chake na familia yake ikiwa ni pamoja na huduma zote zinazotolewa ndani kama kufanya usafi, dawa ya meno, na vifaa vya vyoo, ambayo hukatwa kutoka katika mshahara wake dola 400,000 kila mwaka.
Watu
wengi wanajua kuhusu eneo la Bowling lakini kuna mambo mengine kadhaa
ya kuvutia katika eneo la chini ya White House. Ukiachilia chumba cha
‘situation’ ambacho hutumiwa na rais wa Marekani pindi kunapotokea
dharura ya kitaifa au kimataifa kuna vitu kama duka la maua, karakana ya
mafundi seremala, na ofisi ya daktari wa meno kiasi kwamba rais hana
sababu ya kutoka nje ya White House kwa shida yoyote ile. Kila kitu kimo
ndani ya ikulu ya Marekani.
Ikulu
ya marekani imekuwa ya kushangaza kwa kuwa moja ya taasisi maarufu
duniani. White House kila wiki inapata hadi wageni 30,000 na barua
65,000. Aidha karibu simu 3,500 hupigwa, barua pepe 100,000, na faksi 1000 hupokelewa katika ikulu hiyo ya Marekani kwa wiki.
Pamoja
na ukweli kuwa Ikulu ya marekani hairuhusu kuingilia faragha za Raisi
pamoja na familia yake ambao hutumia simu maalumu bado huwezi kuweka
hakikisho la mia kwa mia kuwa baadhi ya mazungumzo ndani ya ikulu ya
Marekani huvuja.
Ikulu
ya marekani ilijengwa kwa msaada wa watu wengi. wasanii wengi wa Ulaya
na wafanyakazi wahamiaji ikiwa ni pamoja na waashi kutoka Scotland.
Matofali na plasta ilifanywa na wafanyakazi kutoka
Ireland na Italia.
Katika hali ya kusikitisha historia za kumbukumbu za
mishahara zinaonyesha wajenzi wengine walikuwa watumwa wamerekani wenye
asili ya Afrika.
Jina
la White House halikuwa likitumiwa hapo kabla hadi alipoingia
madarakani rais Theodore Roosevelt ndipo ikulu hiyo ikapewa jina hilo.
Awali ikulu hiyo ilijulikana kama kasri la watendaji.
Kama ilivyo kwa majengo yoyote makubwa duniani, mauzauza hayakosekani na miongoni mwa mauzauza hayo kubwa ni lile la rais Winston Churchill kukataa kulala tena katika master bedroom ya Lincoln baada ya mzimu wa Lincoln kumtokea rais Churchill ambapo alimwona ameketi kando ya tanuru chumbani alipotokeza kutoka kuoga.
White
House daima imekuwa katika mabadiliko ambapo awali haikutarajiwa
kuchaguliwa kwa rais mlemavu na ilipotokea ilibidi kurekebisha milango
na kujengwa kwa lifti ili kumwezesha rais mlemavu kutembelea maeneo yote
ya ikulu ikiwa ni pamoja na kujengwa kwa bwawa maalumu la matibabu kwa
rais huyo mlemavu.
Katika
ajabu la kumi na moja rais Clinton alifanya marekebisho ya ikulu ya
aina yake. Yeye alijenga baseni la kuogea lenye maji moto lenye ukubwa
wa kutosha watu saba. Pia kulikuwa na uwezekano wa watu wawili tu
kutumia beseni hilo.
0 comments:
Post a Comment