Monday, May 16, 2016
Kiungo kutoka nchini Ufaransa, N’Golo Kante ameripotiwa kuwa katika
mipango ya kutaka kujiunga na klabu ya Arsenal katika kipindi hiki cha
kuelekea majira ya kiangazi.
Kiungo huyo ambaye ni sehemu ya kikosi cha klabu bingwa nchini
England, Leicester City ameonyesha kuwa na mipango hiyo kutokana na
kuhusishwa na taarifa za kuondoka King Power Stadium baada ya kumaliza
shughuli ya kufikia mafanikio kutwaa taji.
Taarifa zilizochapishwa na jarida la michezo la nchini Ufaransa
liitwalo Le 10 Sport, zimeeleza kwamba, Kante anajipanga kucheza soka
kaskazini mwa jijini London, kutokana na kuwa na ndoto hizo tangu akiwa
na umri mdogo.
Hata hivyo imebainika kwamba Kante mwenye umri wa miaka 25, aliwahi
kusema mbela ya watu wake wa karibu, kwamba endapo itatokea anahitaji
kuachana na The Foxes, atakua radhi kubaki nchini England na kujiunga na
Arsenal.
Maneno hayo yanadaiwa kusemwa na Kante, kufuatia fununu zilizopo za
kuwindwa na baadhi ya klabu za soka barani Ulaya, kutokana na uwezo wake
mkubwa aliouonyesha wakati wa msimu wa 2015-16 ambao ulifikia tamati
hapo jana.
Mbali na klabu ya Arsenal kuonyesha kuwa tayari kumsajili Kante,
klabu nyingine zinazotajwa kuwa katika mawindo ya kuiwania saini ya
kiungo huyo ni Chelsea pamoja na Real Madrid.
Related Posts
Donny Roberty Mshindi Miss Mwanza 2016 Tazama Picha hapa chini.
Usiku wa jana Ijumaa Agost 19,2016 kuamkia leo Jumamosi Agost 20,20...
MAONESHO YA BIASHARA ROCK CITY MALL MWANZA.
Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda n...
TFF Yatoa Angalizo Kwenye Msimu Mpya Wa VPL 16-17.
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/17 inatarajiwa kuan...
Sumatra Imesema hakuna usafiri utakaositishwa.
MAMLAKA ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imewatoa hofu ...
Hesabu inaendelea Ibra aweka mbili Nyumbani (VIDEO).
Endeleeni kuhesabu, ndiyo lugha rahisi unayoweza kuitumia baada...
Mambo 8 Yatakayokusaidia Kufikia Malengo Yako.
Kila wakati wengi wetu katika maisha, ni watu wa kujiwekea malengo....
Mkurugenzi Atishia Kuitisha Daftari la Mahudhurio saa tisa Usiku sababu Je?
Normal 0 false false false EN-U...
Gwajima atiwa Nguvuni na Polisi Dar, Imekuaje?
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limemkamata ...
Baada ya Cameroon huyu ndio kuwa Waziri mkuu wa Uingereza.
Katika saa au siku kadhaa zijazo, Waziri wa maswala ya nda...
ULIPITWA; MATOKEO YA ENGLAND VS RUSSIA YAKO HAPA.
June 11 2016 michuano ya Euro 2016 inayofanyika Ufaransa imeen...
- Blogger Comments
- Facebook Comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment