Yusufu amejibu upya swali lililomponza bosi wake wa zamani, Charles Kitwanga. Uamuzi wa
kurudia swali hilo ulitolewa juzi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisema swali
hilo lilijibiwa katika hali ya ulevi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na
wabunge wakaomba mwongozo kuhusu majibu yaliyotolewa.
Kitwanga aliondolewa katika nafasi yake na Rais John Magufuli
baada
ya kujibu ya swali hilo akiwa amelewa.
Leo, Masauni amejibu swali hilo namba 211 la Mbunge wa Viti Maalumu
Devota Minja (Chadema) na kuonyesha utofauti mkubwa kati ya majibu yake na
yale yaliyotolewa mwishoni kuongea kwa ulevi mwa wiki na aliyekuwa Waziri wake.
Swali hilo ambalo awali lilikuwa namba 205, liliulizwa na Devota Minja akitaka kujua Serikali ina mpango
gani wa kuboresha makazi ya polisi na askari magereza wanaoishi katika
nyumba chakavu zisizokuwa na hadhi ukilinganisha na kazi zao kwa
jamii.
Nyakati zote hizo, swali hilo limeulizwa na wabunge tofauti wa
Chadema
kutokana na Minja kutokuwapo, mara ya kwanza likiulizwa na Suzan Kiwanga
(Mlimba) na leo Joseph Selasini wa Jimbo la Rombo.
Tofauti ya majibu ya Kitwanga, Masauni ametoa takwimu katika
ujenzi wa nyumba 9,500 za Magereza nchi nzima, lakini kwa upande
wa nyumba za Polisi majibu yalikuwa yaleyale.
Tazama video ya majibu ya Naibu waziri hapa chini
0 comments:
Post a Comment