Moja ya changamoto kubwa ya kushindwa kufanikiwa ni kutokujua unataka nini katika Maisha yako. Huenda ukawa haujanielewa ngoja nikueleweshe, ni hivi unakuta mtu anaona maisha hayaendi vizuri mwisho wa siku ukimuuliza mtu huyo anataka kufanya nini, bila shaka kwa kuwa mtu huyo hajui kile anachokitaka atakwambia kazi yeyote ile mimi nafanya.
Ukiangalia juu ya kauli hiyo ni sawa, mtu huyo huenda akawa sawa hii ni kutokana na hali yake aliyonayo. Lakini katika kanuni ya kimafanikio hakuna majibu ya kusema unataka kufanya chochote kile. Ila ni lazima ujue unataka kufanya nini. Moja ya majonzi ya watu waliofeli kimaisha ni kwamba walichanganya vitu vingi kwa wakati mmoja.
Tujifunze kitu kupitia hadithi ifuatavyo.
Hapo zamani za kale kulikuwepo na mfugaji fulani katika kijiji fulani. Na mfugaji huyo alijipatia umaarufu mkubwa sana kijinini hapo hii ni kutokana alivyobobea katika shughuli hiyo, na kutokana na umaarufu huo aliweza kulinda heshima ya jina lake na kuongeza idadi kubwa ya mifugo.
Kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo na mifugo ilivyozidi kuongezeka miaka na miaka, hata hivyo kama ilivyo kwa jongoo kuwa na miguu mingi bila macho ni sawa na bure hivyo ndivyo ilivyotokea kwa mfugaji huyo kutokana na ufugaji hakutaka hata siku moja kumuuza hata mnyama mmoja kwa sababu aliweka malengo yake ya muda mrefu na kuamini ipo siku atakuja kuwa na pesa nyingi na kuwa tajiri mkubwa zaidi kijijini hapo.
Acha kuwa na tamaa na mipango mingi, itakukwamisha.
Hata hivyo kutokana imani hiyo aliyokuwa nayo furaha na umarufu uligeuka kilio na majonzi hasa pale ulipo ingia ugonjwa wa bonde la ufa (Rift valley) kijijini hapo. Ugonjwa huo uliweza kuangamiza idadi kubwa ya wanyama aliowamiliki mpaka akabakiwa na ng'ombe mmoja.
Mfugaji alinung'unika sana lakini alimbidi akubaline na hali hiyo ambayo imetokea. Hivyo akaamua kumuhudumia yule ng'ombe kama mtoto wake kwani kila alichokihitaji ng'ombe yule alikipata kutoka kwa mfugaji huyo. Hayo ndiyo yalikuwa maisha ya mfugaji na ng'ombe yalivyokuwa.
Soma; Hiki Ndicho Kitu Kinachokufanya Ushindwe Mara Kwa Mara Katika Maisha Yako.
Siku moja alfajiri mfugaji aliamua kwenda na ng'ombe wake sehemu ambayo ng'ombe yule alikunywa maji kama ilivyokuwa ratiba ya mfugaji yule kila siku. Wakati wanaelekea katika eneo hilo ghafla mbele aliona kiatu, kiatu ambacho kilikuwa ni kizuri sana, aliamua kukichukua kiatu kile na kukiangalia na kuona kinamtosha vizuri baadae ilishangaa mbona kiatu kizuri kiasi kilikuwepo pale barabarani wakati anajiuliza hayo aling'aza macho yake huku na huko lakini hakuona kiatu kingine cha mguu mwingine.
Kwa kuwa hakuona kiatu kingine aliamua kuachana na kiatu kile na kuondoka na ng'ombe wake. Mfugaji aliendelea na safari yake kwa mwendo mrefu sana lakini kadri alivyozidi kwenda ghafla alikutana na kiatu kingine cha mguu mwingine ambacho kinafanana na kile alichokiacha awali. Mfugaji alifurahi sana hivyo aliamua akiache kiatu kile cha pili pamoja na ng'ombe mahali pale na kurudi kwa kasi sana kwenda kuchukua kiatu kingine.
Lakini cha ajabu kilichomkuta ni kwamba baada ya kwenda mahali pale kilipokuwepo kiatu cha mwanzo hakukiona kiatu kile, alijaribu kukitafuta sana kiatu kile lakini hakukipata hivyo aliamua kurudi mwanzo ambako aliamuacha ng'ombe na kiatu cha pili lakini cha kushanganza ni kwamba hata huko hakumkuta ng'ombe wala kiatu kile. Mfugaji alilia sana kwa sababu alimpoteza ng'ombe wake ambaye alibaki mmoja na aliyempenda sana. Mwisho wa siku alikosa vyote.
TAFSIRI YA HADITHI HII NI NINI?
Tafsiri ya hadithi hii ni kwamba watu wengi ni wazuri wa kimawazo na kuchangamkia fursa mbalimbali ila changamoto kubwa inakuja hasa pale ambapo unataka mafanikio ya haraka hivyo unajikuta unaingia katika sakata la kuchanganya mambo mengi kwa wakati mmoja. Mwisho wa siku unajikuta unafanya kitu hiki unaacha mara unafanya kitu kingine kama alivyofanya mfugaji na mwisho wa siku akajikuta anakosa yote.
Hivyo ni
wakati muafaka leo wa kujua unataka kufanya nini na kukimalisha na sio
kuwa na maisha yakutaka mambo mengi kwa pupa pupa na mwisho kukosa
vyote. Kuwa mtu chanya ili kupata mafanikio ya kweli.
Nukuu ya Leo inasema; Ukijua kilichomo ndani yako wewe ni tajiri.
Nukuu ya Leo inasema; Ukijua kilichomo ndani yako wewe ni tajiri.
0 comments:
Post a Comment