Jeshi la Polisi
mkoani Ruvuma linamshikilia mkazi wa eneo la Bombambili, Manispaa ya Songea kwa
tuhuma za kukutwa akimbaka mtoto wa miaka saba anayesoma darasa la pili.
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Ruvuma, Zuber Mwombeji alisema mtuhumiwa alitenda kosa hilo Mei 18
mwaka huu saa 11 jioni nyumbani kwao na mtoto huyo.
Alifafanua kuwa siku
ya tukio mkazi huyo alikwenda sehemu hiyo kuangalia runinga sebuleni na baada
ya muda mfupi binti huyo alirejea nyumbani akitokea shule.
“Msichana
huyo alikuja sebuleni kuangalia runinga wakati huo wafanyakazi wa ndani wa
nyumba hiyo walikuwa nje na ndipo kijana alipopata mwanya wa kufanya ukatili
huo,” alisema kamanda.
Alisema baada ya muda
mfupi kupita, mfanyakazi wa kike aliingia sebuleni ghafla na kumkuta akimbaka
mtoto huyo.
Alifunga mlango,
kisha aliwaita majirani na viongozi wa Serikali wa mtaa huo.
Kamanda alisema
wananchi walimkamata mtuhumiwa na kumpeleka polisi. Pia, mtoto huyo
alichunguzwa na madaktari walithibitisha kuwa aliingiliwa kimwili na kuharibiwa
sehemu zake za siri.
Jeshi
la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia mkazi wa eneo la Bombambili,
Manispaa ya Songea kwa tuhuma za kukutwa akimbaka mtoto wa miaka saba
anayesoma darasa la pili.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Zuber Mwombeji alisema mtuhumiwa alitenda
kosa hilo Mei 18 mwaka huu saa 11 jioni nyumbani kwao na mtoto huyo.
Alifafanua
kuwa siku ya tukio mkazi huyo alikwenda sehemu hiyo kuangalia runinga
sebuleni na baada ya muda mfupi binti huyo alirejea nyumbani akitokea
shule.
“Msichana
huyo alikuja sebuleni kuangalia runinga wakati huo wafanyakazi wa ndani
wa nyumba hiyo walikuwa nje na ndipo kijana alipopata mwanya wa kufanya
ukatili huo,” alisema kamanda.
Alisema baada ya muda mfupi kupita, mfanyakazi wa kike aliingia sebuleni ghafla na kumkuta akimbaka mtoto huyo.
Alifunga mlango, kisha aliwaita majirani na viongozi wa Serikali wa mtaa huo.
Kamanda
alisema wananchi walimkamata mtuhumiwa na kumpeleka polisi. Pia, mtoto
huyo alichunguzwa na madaktari walithibitisha kuwa aliingiliwa kimwili
na kuharibiwa sehemu zake za siri.
- See more at: http://edwinmoshi.blogspot.com/2016/05/jamaa-akutwa-laivu-akimbaka-mtoto-wa.html#sthash.A5byMr7l.dpuf
0 comments:
Post a Comment