Inaaminika kuwa deal hiyo na raia huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 53 ilikubaliwa kabla ya ushindi wa United kwenye fainali ya kombe la FA dhidi ya Crystal Palace Jumamosi.
Ikiwa United imeshindwa kufuzu kushiriki kombe la mabingwa wa Ulaya
chini ya kocha wake wa sasa, Louis van Gaal, uongozi wa Old Trafford
unafikiriwa kuamua kufanya mabadiliko yanayohitajika.
Mourinho amekuwa benchi tangu atimuliwe na Chelsea December mwaka jana.
Klabu hiyo imepanga kutangaza ujio wake mapema wiki ijayo baada ya kumwambia Van Gaal, 64, afungashe virago vyake.
Kocha huyo raia wa Uholanzi bado ana msimu mmoja kwenye mkataba wake
wa miaka mitatu na licha ya kutumia paundi milioni 250 kusajili
wachezaji wapya, ukocha wake umewaangusha mashabiki wengi kwa timu yake
kumaliza katika nafasi ya nne na kisha ya tano kwenye ligi kuu ya
England katika misimu miwili aliyoifundisha.
Mourinho alikuwa kwenye mchezo wa masumbwi Jumamosi hii ambapo bondia
David Haye alishinda lakini alikataa kuongea chochote iwapo anaenda
kumrithi Van Gaal.
Mourinho ni mmoja wa makocha waliofanikiwa zaidi huku akishinda
vikombe vitatu akiwa na Chelsea, pamoja na kuingoza Porto na Inter
Milan kwenye ushindi wa ligi ya mabingwa mwaka 2004 na 2010.
Aliwahi pia kuwa kocha wa Real Madrid na kuiwezesha kushinda kombe la Spanish La Liga mwaka 2012.
0 comments:
Post a Comment