Kiungo kutoka nchini Kenya, Victor Wanyama ameugomea uongozi wa klabu
ya Southampton katika suala la kusaini mkataba mpya, kwa kushinikiza
kuondoka klabuni hapo.
Wanyama amefanya maamuzi hayo, huku ikifahamika aliyekua meneja wa
The Saint, Mauricio Pochettino anahitaji kuona akikamilisha harakati za
kumsajili wakati wa dirisha la usajili ili wawe wote Tottenham Hotspurs.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, amesaliwa na mkataba wa mwaka
mmoja wa kuitumikia klabu ya Southampton ambayo ilimsajili akitokea
Celtic mwaka 2013, kwa ada ya Pauni milioni 12.5.
Kutokana na hatua hiyo uongozi wa The Saint, kwa sasa unasubiri ofa
yoyote itakayomlenga kiungo huyo na tayari wameshaweka wazi thamani yake
kwa kutaja kiasi cha Pauni milioni 25.
Klabu bingwa nchini England Leicester City, pia inatajwa kuwa katika
mlolongo wa kutuma ofa St Mary’s, ili kuangalia uwezekano wa kumsajili
Wanyama.
Wanyama, anapigiwa upatu wa kusajiliwa huko King Power Stadium, ili
kuwa sehemu ya mbadala wa kiungo kutoka nchini Ufaransa N’Golo Kante
ambaye amegoma kusaini mkataba mpya.
0 comments:
Post a Comment