Rais John Magufuli ametoa salamu za
pole kwa wakazi wa mkoa wa Mwanza, kutokana na mauaji ya watu watatu, waliouawa
kwa kukatwa mapanga wakiwa msikitini
Taarifa
iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, jijini Dar es Salaam jana,
ilisema Rais Magufuli amesema yupo pamoja na wakazi wa mkoa huo wa Mwanza
katika kipindi hiki cha majonzi, kuomboleza watu hao na pia alisema anawaombea
wale waliojeruhiwa wapone.
Wakati
huo huo, Wizara ya Mambo ya Ndani imesema imesikitishwa na mauaji ya watu hao
watatu, waliouawa msikitini katika wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Kauli
hiyo ya Serikali, ilitolewa bungeni mjini Dodoma jana na Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Masauni Yussuf Masauni.
Masauni
alisema kuwa Serikali inawapa pole wakazi wa Mwanza, viongozi wa mkoa na wilaya
ya Nyamagana na mbunge wa jimbo hilo, Stanslaus Mabula.
Taarifa
iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, jijini Dar es Salaam
jana, ilisema Rais Magufuli amesema yupo pamoja na wakazi wa mkoa huo wa
Mwanza katika kipindi hiki cha majonzi, kuomboleza watu hao na pia
alisema anawaombea wale waliojeruhiwa wapone.
Wakati
huo huo, Wizara ya Mambo ya Ndani imesema imesikitishwa na mauaji ya
watu hao watatu, waliouawa msikitini katika wilaya ya Nyamagana mkoani
Mwanza.
Kauli hiyo ya Serikali, ilitolewa bungeni mjini Dodoma jana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Masauni Yussuf Masauni.
Masauni
alisema kuwa Serikali inawapa pole wakazi wa Mwanza, viongozi wa mkoa
na wilaya ya Nyamagana na mbunge wa jimbo hilo, Stanslaus Mabula.
- See more at: http://edwinmoshi.blogspot.com/2016/05/rais-magufuli-atoa-machozi-kufuatia.html#sthash.9sYQEgt6.dpuf
0 comments:
Post a Comment