728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, May 21, 2016

    STORI KUBWA MWANZA NI JEMBEKA FESTIVAL 2016, MAPOKEZI YA MSANII NEYO JIJINI MWANZA NI HATARI.

    Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo jana akiondoka katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kiliamanjaro kueelekea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa safari ya jiji Mwanza kutumbuiza kwenye Jembeka Festival 2016. Kulia ni Meneja wa Hoteli hiyo, Timothy Mlay.

    Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani Neyo amewasili jijini Mwanza jana jioni akitokea Dar es Salaam na kupokelewa na umati mkubwa wa wakazi wa jiji hilo kama Mfalme katika Uwanja wa Ndege wa jijini Mwanza.

    Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania ndio wadhamini wakuu wa Jembeka Festival 2016 kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Fastjet, SYSCORP Cooperation, CF Hospitals, KK Security, Samsung, EF Outdoor, Lacairo Hotel, Ndege Insurance, Jembe Media Group pamoja na Coca Cola.

    Msanii huyo anatarajiwa kutumbuiza leo katika tamasha hilo kwa kupiga 'Live Music' katika uwanja wa CCM Kirumba ambapo msanii wa kimataifa kutoka nchini, Diamond Platnumz, FID Q, Stamina, Mr. Blue, Ney wa Mitego, Maua Sama, Rubby, Baraka Da Prince, Juma Nature, MO Music na wengine wengi watapanda jukwaa moja na msanii Neyo.
    Picha zaidi hapa chini.











    Imeandaliwa na Zainul Maige
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: STORI KUBWA MWANZA NI JEMBEKA FESTIVAL 2016, MAPOKEZI YA MSANII NEYO JIJINI MWANZA NI HATARI. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top