728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, May 24, 2016

    Yanga kundi moja na TP Mazembe ya kina Ulimwengu.


    Yanga SC imepangwa kundi la A katika Kombe la Shirikisho Afrika pamoja na mabingwa wa zamani barani, TP Mazembe ya DRC, MO Bejaia ya Algeria na Medeama ya Ghana.

    Klabu ya Yanga ilifanikiwa kuishusha timu ya Sagrada Esparenca ya Angola bao 2-1 na kufuzu kwenye hatua ya makundi ya michuano ya CAF kwa mara ya kwanza tangu walipofanikiwa kufanya hivyo kwa mara ya kwanza na ya mwisho mwaka 1998.

    Yanga iliangukia katika kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Shirikisho, baada ya kutolewa na Al Ahly ya Misri katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 3-2, ikilazimishwa sare ya 1-1 Dar es Salaam na kufungwa 2-1 kule Misri.

    Kundi B linaundwa na timu za Kaskazini mwa Afrika tupu ambazo ni Etoile du Sahel ya Tunisia ambao ni mabingwa watetezi, Ahly Tripoli ya Libya, FUS Rabat na Kawkab zote za Morocco.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Yanga kundi moja na TP Mazembe ya kina Ulimwengu. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top