728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, May 31, 2016

    Aunt Ezekiel:Ndoto yangu ni kuwa na watoto watatu.


    Msanii wa filamu za Bongo Movies Aunt Ezekiel amesema anatamani kupata watoto mapacha ili akamilishe ndoto yake ya kuwa na watoto watatu.

    Aunt amesema kuwa baada ya Mungu kumjalia kupata mtoto mmoja,sasa dua zake anazoomba ni kupata mapacha na hapo atakuwa ametimiza idadi ya watoto aliokuwa anawahitaji.

    “Kwanza kabisa ninamshukuru Mungu kwa kunijalia kuwa na familia,sasa ninatamani kupata watoto mapacha ili nitimize idadi ya watoto watatu,idadi hiyo ninaweza kuwalea na kuwatunza vizuri,” alisema Aunt.

    Msanii huyo alisema mtu amepanga idadi ya watoto anaotaka kuzaa kulingana na uwezo wake kimaisha,na kwamba yeye ana uwezo wa watatu.

    Mtoto wa kwanza wa msanii huyo anayeitwa Cookie amenaza na Moses Iyobo ambaye ni dansa wa Diamond.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Aunt Ezekiel:Ndoto yangu ni kuwa na watoto watatu. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top