728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 15, 2016

    Kalapina Amesema Majigambo yanaleta bifu kwenye mziki wa Hip Hop.


    Rapper mwenye harakati Kalapina amezungumzia sababu ya kuwepo kwa bifu za mara kwa mara kwa wasanii wa Hip Hop.

    kalaPina amesema sababu kubwa inayopelekea kuwepo kwa bifu kati ya wasanii wa Hip Hop ni aina ya muziki wanaoufanya, ambao unakuwa wa majigambo sana.

    “Bifu sehemu zote zipo, inategemea tu hiyo bifu imepata nafasi gani kwenye vyombo vya habari, kwenye hip hop inakuwa sana kwa sababu kwenye rap music kuna majigambo, kujisifia sifia sasa kwenye majigambo unaweza ukajisifia sana ukamkandya mtu mwengine, na yeye inabidi atoe ngoma akukandye wewe, vitu kama hivyo ndio vinazalisha bifu na wakati mwengine inakuwa ya ukweli kabisa”, alisema Kalapina.

    Kalapina kwa sasa ambaye ametoa wimbo wake unaoitwa 'wanaiga iga', anaendeleza harakati za kupambana na madawa ya kulevya, ambayo hivi karibuni alinukuliwa akisema wasanii wanaiga sana na kufikia hatua ya kujiingiza kwenye matumizi ya madawa hayo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Kalapina Amesema Majigambo yanaleta bifu kwenye mziki wa Hip Hop. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top