728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, May 26, 2016

    UKO TAYARI KWA UJIO WA ALBAM YA MKE NA MUME,SUPRISE VERY SOON!!


    KUMEKUA na maneno mengi mtaani kwamba baada ya albam ya Beyonce ‘Lemonade’ kuachiwa na ikawa kama ina maelezo ya kumchana mume wake kwa suala la kutokua muaminifu kwenye ndoa, pia zikatoka taarifa kwamba Jay Z naye anakuja na albam yenye majibu juu ya Lemonade.

    Sasa kama ulikua unasubiria hilo umefeli, issue ni kwamba wanandoa hawa wanatarajiwa kutoka na albam ya pamoja hivi karibuni!

    Page Six wameripoti kuwa Bey na Jay! Wamekamilisha albam yao na soon itaachiwa kupitia mtandao wa Tidal ambao unamilikiwa na wasanii hao pia.

    Wapenzi hawa wanaotajwa kuwa na ndoa inayowaingizia mkwanja mrefu zaidi kwasasa, wameripotiwa kurekodi albam hiyo kwa siri sana kwa lengo la kuiachia mwezi huu au mwezi ujao mapema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: UKO TAYARI KWA UJIO WA ALBAM YA MKE NA MUME,SUPRISE VERY SOON!! Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top