728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 27, 2016

    BAADA YA KUJIRUSHA KUTOKA KWENYE MNARA WA SIMU KILICHOMKUTA NI HIKI.



    Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la PAULO PASCHAL mwenye umri wa miaka 40 Mkazi wa magu Mkoani Mwanza amenusurika kifo baada ya kujirusha kutoka katikati ya mnara wa simu uliopo barabara ya makongoro-Airpot jijini Mwanza.

    Akijibu swali kwanini amepanda juu ya mnara Huo na kutaka kujiua akiwa katika hospitali ya sekour Toure bwana Paulo paschal amesema alilazimika kufanya hivyo kutokana na Jeshi la polisi kushindwa kusikiliza kesi zake kama mtuhumiwa sambamba na hilo amesema usiku wa kuamkia leo baadhi ya watu  waliokuwa wakimfukuza kwa lengo la kutaka kumuuwa hivyo katika hatua ya kujinusuru alilazimika kuingia katika mnara huo.

    Mashuhuda wa tukio wamesema huenda kijana huyo amefikia maamuzi hayo kutokana na ugumu wa maisha ambao amekuwa akiulalamikia huku wengine wakisema ni kutokana na kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya ambayo amekuwa akiyatumia.

    Kwa upande wake HERIETS MADAKTA Muuguzi wa zamu ambaye amempokea bwana Paulo katika hospitali ya mkoa Sekour Toure amesema bwana PAULO hana mvunjiko wowote katika mwili  tofauti na michubuko katika mwili wa kijana huyo.

    Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa jeshi la uokoaji na zima moto mkoani Mwanza, Kaimu kamanda wa jeshi la Hilo Mussa Kaboni, ametoa rai kwa makampuni yenye minara ya simu kuimarisha ulinzi katika minara hiyo ili kuondoa hatari inayoweza kujitokeza kutoka kwa raia wasio wema.

    Aidha Zoezi la uokoaji lilichukua zaidi ya masaa sita likianza saa Tatu asubuhi mpaka saa sita mchana.

    Picha zaidi Hapa chini.













    Picha na Binagamediablog.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BAADA YA KUJIRUSHA KUTOKA KWENYE MNARA WA SIMU KILICHOMKUTA NI HIKI. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top