728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, May 18, 2016

    Madee: Ningekuwa bado nafanya Hip Hop kama zamani ningekuwa tayari nmeshapotea.


    Msanii wa muziki kutokea Tip Top Connection Madee, amesema angeendelea kudumu na staili yake ya kurap kama zamani, mpaka sasa angekuwa amekwisha potea kwenye ‘Game’ na ulimwengu wa muziki tayari.

    Madee ameiambia Times Fm kuwa, watu wanataka mabadiliko katika muziki na tayari muziki umekuwa biashara kubwa sana.

    “Watu wanataka changes, kama biashara haikulipi kwanini uendelee kufanya inakuingizia hasara kila kukicha, ningekuwa narap mpaka leo nisingekuwepo kwenye game ningepotea, dunia yenyewe inabadilika sasa kwa nini wewe usibadilike” alisema Madee.

    Katika hatua nyingine msanii huyo ametoa mtazamo wake kwa nini muziki wa Hip Hop haufanyi vizuri nyumbani kama zamani, amedai Hip Hop inapendwa na kundi la ‘wahuni’ wachache na machizi mtaani ambao ni ngumu kwenda dukani kununua kazi anayoipenda.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Madee: Ningekuwa bado nafanya Hip Hop kama zamani ningekuwa tayari nmeshapotea. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top