728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, May 25, 2016

    Haya Ndio Mambo ya kuepuka kabla ya kuoa Kutoka Kwa Sheikh Mussa Salum.


    Sheikh amebainisha kwamba mwanamume akioa kwa sababu tuu ya uzuri wa mwanamke uzuri unaweza ukapotea muda wowote, mtu akioa kwa sababu ya mali au umaarufu nao unaweza kuisha wakati wowote na mtu hawezi kuwa mwema kutokana na vitu hivyo.

    Sheikh ameyabainisha hayo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha SUPAMIX kinachorushwa na kituo cha redio cha East Afrika Radio jijini Dar es salaam jana.

    Ameweka wazi kwamba kinachotakiwa kwa mwanamume kuangalia kabla ya kuoa ni jambo kubwa moja 'Dini' ambapo hii ndiyo huonyesha kama mtu anafuata sheria na kuwa na hofu ya Mungu.

    Aidha amesisitiza kwamba na mwanamke anapaswa kuangalia aolewe na mtu ambaye ana maadili na Dini hapo ndipo ndoa inaweza kudumu.

    Hata hivyo Sheikh ameweka bayana kwamba Mwenyezi Mungu hapendi mtu wa kuoa na kuacha kwa sababu ndoa imewekwa na mwenyezi Mungu na ndiyo maana mtu huwa na muda wa kutulia kwanza kabla ya kufanya maamuzi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Haya Ndio Mambo ya kuepuka kabla ya kuoa Kutoka Kwa Sheikh Mussa Salum. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top