728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 27, 2016

    Kama Upo single? mambo ya kufanya kabla hujaingia tena kwenye mahusiano.


    Mapenzi yanaumiza sana, na kabla hujaanza kuwaza kumtokea msichana mwingine au wewe dada kumkubali Yule mshikaji alikuwa anakufwatilia kwa mwaka sana, fanya haya yafwatayo.

     Jipende kuliko Kawaida


    Tumia muda huu ambao uko single na ujipende  zaidi kuliko ulivyokuwa katika mahusiano, muda wa kujiwaza wewe, kula vizuri, vaa vizuri, pata muda mwingi wa kupumzika, tembelea sehemu za starehe mwenyewe bila kuwaza kutafuta mtu mwingine na utajifunza kitu.

    Kuna na Marafiki wa jinsia tofauti na wewe

    Jichanganye na marafiki wa jinsia tofauti na wewe na ujifunze mambo ya mahusiano kupitia kwao, toka nao matembezini au sehemu za michezo ila usianze mahusiano mapema  kama hauko tayari.

    Kuwa Karibu na Ndugu zako


    Huwezi jua ni kwa kiasi gani umekaa mbali na watu wako wa karibu wakati ukiwa uko busy na mpenzi wako. Wakati kama huu utumie kutoka na ndugu zako wa karibu au kushinda nyumbani mwisho wa wiki, pamoja na familia yako.

    Fanikisha Ndoto zako

    Ukiwa katika mahusiano kila kitu lazima kiwe kwa ajili ya wote wawili ila kama upo single ni raisi kufanya kitu kwa ajili yako mwenye na tumia muda huu kufanikisha ndoto zako, fikiria malengo yako zaidi ili ufanikiwe.

    Tafakari nini unataka kwenye Mahusiano Mengine
    Tumia huu muda, kuangalia ni aina gani ya mpenzi unamuhitaji na nini kitakupa furaha kutoka kwake, ila pia tambua furaha kama haipo kwako huwezi tegemea kuipata kwa binadamu mwingine. Kwahiyo jua ni jinsi gani utakuwa na furaha  bila kutegemea mapenzi au kuwa na mpenzi.

    Fanya kitu kipya

    Kama kufuga mbwa ,paka au chochote ambacho hujawahi fanya hakikisha haukosi cha kufanya ili usiwe mpweke, Tembelea mbuga za wanyama au nenda nchi nyingine kama una uwezo na jifunze vitu vipya.

    Jenga ukaribu na Marafiki zako

    Inasemekana kuwa marafiki wengi hupoteana au huwa hawana tena mazoea ya karibu pindi wanapoanza mahusiano, angalia umeshakuwa mbali na marafiki zako wangapi toka uanze mahusiano na jenga tena urafiki na watu wako.

    Zingatia kusubiri kabla hujaanza mahusiano mapya, unaweza kujiingiza kwenye mahusiano mengine ambayo yatakuwa matatizo kuliko ulipotoka na ukajikuta unajutia maamuzi yako.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Kama Upo single? mambo ya kufanya kabla hujaingia tena kwenye mahusiano. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top