728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 20, 2016

    Ujumbe Wa Zitto Kabwe baada ya Rais Magufuli kumfuta kazi Charles Kitwanga



    Stori kubwa ambayo imeingia kwenye headlines jioni ya May 20 2016 lakini pia inatarajiwa ndio itakaa katika kurasa za mbele za magazeti ya kesho May 21 2016, ni kuhusu uamuzi wa Rais Magufuli kumfuta kazi aliyekuwa waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga kutokana na kuingia bungeni akiwa amelewa.

    Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe ametumia ukurasa wake wa facebook kuandika mtazamo wake baada ya Rais Magufuli kufanya maamuzi hayo ya kumfuta kazi waziri Kitwanga.


    “Uamuzi wa Rais kumfukuza kazi Waziri wa Mambo ya Ndani unatuma ujumbe mmoja – hataki mchezo. Rais amethibitisha kuwa anao uwezo wa kutumbua hata aliowateua. Ni maamuzi muhimu sana kwa Kiongozi wa aina yake. Wale vijana waliokuwa wanatumwa kumtetea wasimame kumtetea. Rais kaonyesha Uongozi ‘ no nonsense “
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Ujumbe Wa Zitto Kabwe baada ya Rais Magufuli kumfuta kazi Charles Kitwanga Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top