728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 27, 2016

    Haya maneno Mazito kutoka kwa Rais Magufuli Yawaendee wala Rushwa.


    Rais John Magufuli jana alituma ujumbe mzito katika mapambano dhidi ya rushwa nchini, akisema mapambano hayo ndiyo mwelekeo wake na hatabadilika hata kama itakuwa ni kutoa sadaka mwili wake.

    Alitoa ujumbe huyo alipofungua mkutano wa wakandarasi jijini Dar es Salaam, akiendelea na ‘kampeni yake’ ya kuhimiza uzalendo na kupambana na ufisadi.

    “Na bahati nzuri nashukuru, Watanzania wananiombea na Mungu ananisimia kwa sababu nafahamu kazi hii zikupewa na mtu, nilipewa na Mungu,” alisema Rais huku akipigiwa makofi.

    “Na watu wanaoteseka ni watu wa Mungu, hasa watu maskini. Ni lazima nitimize wajibu wangu, hata kama ni kwa kutoa sadaka yangu, sadaka ya mwili wangu.”

    Magufuli hakuwa anapewa nafasi ya kupitishwa na CCM kuwania urais, lakini upepo ulibadilika ghafla baada ya jina la Edward Lowassa kukatwa na kubakia makada watano.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Haya maneno Mazito kutoka kwa Rais Magufuli Yawaendee wala Rushwa. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top