728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 20, 2016

    TCRA BADO INAKUKUMBUSHA KUHAKIKI SIMU YAKO KABLA YA 16 JUNE.


    Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), imeendelea kuwakumbusha watumiaji wa simu za mkononi kuhakiki simu zao kabla mamlaka hiyo haijazima simu bandia ifikapo Juni 16 mwaka huu.
    Akizungumza kwenye semina ya wadau wa mawasiliano wakiwemo wauzaji wa simu, Mafundi wa simu, wanahabari pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama, Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungi, amesema takwimu za mpaka mwezi Machi mwaka huu, zinaonesha kuwa asilimia tatu ya simu zinazotumika nchini ni bandia.

    Amesema asilimia 13 ya simu zote nchini ni zile zilizonakilishwa na kwamba idadi ya simu hizo zilizonakilishwa imepungua kutoka asilimia 30 kutokana na elimu inayoendelea kutolewa na TCRA.
    Ametanabaisha kwamba simu bandia zimekuwa zikiingizwa nchini na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu ambao wamekuwa wakitoa punguzo kubwa la bei kwa wateja wanaonunua simu hizo na hivyo kuwahamasisha watu wengi kununua simu bandia.

    Uchunguzi uliofanywa na TCRA umebaini kuwa wastani wa bei ya simu halali kwa Tanzania ni kati ya shilingi elfu 20 hadi elfu 60, bei ambayo wananchi wengi wanao uwezo wa kununua simu halali hivyo waachane na matumizi ya simu bandia kwani zina madhara makubwa.

    Kujua ikiwa simu yako ni halali, unapaswa kutuma nambari za simu yako (IMEI Namba) kwenda 15090 ambapo utapokea ujumbe mfupi wa maneno ukikujulisha ikiwa simu yako ni bandia (fake) ama halali (Orginal) hii ikiwa ni bure kwa watumiaji wa mitandao yote.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TCRA BADO INAKUKUMBUSHA KUHAKIKI SIMU YAKO KABLA YA 16 JUNE. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top