728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 13, 2016

    CAF Yaongeza Makundi Kutoka Mawili Hadi Kufikia Manne



    Shirikisho la Soka Afrika limeongeza idadi ya timu za kuingia hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho kutoka nane za makundi mawili hadi 16 za makundi manne kuanzia mwaka ujao.

    Hayo yamesemwa na Rais wa CAF, Issa Hayatou katika hotuba ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa shirikisho hilo jana Mexico City nchini Mexico.

    Katika mkutano huo uliohudhuriwa na Rais wa FIFA, Gianni Infantino, aliyeongozana na magwiji wa soka, Samuel Eto’o Fils, Luis Figo, Zvonimir Boban, Hayatou alisema mfumo huo utaanza mwakani.

    Mfumo wa sasa wa makundi mawili ya timu nne kila moja, washindi wawili wa kila kundi hutinga Nusu Fainali na baadaye timu zinazoshinda kukutana fainali.

    Wazi katika mfumo mpya wa makundi manne, kila kundi litatoa timu moja ya kwenda Nusu Fainali.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CAF Yaongeza Makundi Kutoka Mawili Hadi Kufikia Manne Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top