728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 15, 2016

    Si kila mtu anaandika mashairi mazuri, Wakazi Ametoa Sababu Hapa.


    Kwenye Exclusive Interview na Metro fm kupitia kipindi cha Friday Club Mix, Rapper Wakazi ametoa sababu kubwa ya baadhi ya wasanii kuandikiana nyimbo, kitendo ambacho kwenye muziki wa bongo fleva bado ni  changamoto.
     
    Wakazi amesema wasanii huwa wanaandika nyimbo za wasanii wengine kwa sababu sio kila mtu ana uwezo au kipaji cha kuandika mashairi mazuri, na kufikisha ujumbe mzuri kwa jamii.

    “Sio kila mtu anauwezo wa kuandika nyimbo, au kusema kwamba a good song writer, ujue kuna watu wana mkono mzuri ambao yeye akiandika mashairi yanamgusa mtu kwa haraka zaidi, na ujumbe unaweza ukakubalika na asilimia kubwa ya watu wanaokusikiliza kwa haraka, na mapema ukawa na impact na jamii nzima”, alisema Wakazi.

    Wakazi ambaye ni rapper anayewania tuzo za KORA mwaka huu, amesema yeye binafsi ni mwandishi mzuri wa mashairi, hivyo hamsumbui kwenye uandishi wa nyimbo zake.

    “Mi naandika mashairi yangu mwenyewe na ni kwamba nikiandika mashairi yangu yanawagusa watu”, alisema Wakazi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Si kila mtu anaandika mashairi mazuri, Wakazi Ametoa Sababu Hapa. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top