728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 13, 2016

    Fahamu Kiasi Ambacho Mpenzi wake Gigy kama hana kabisa Pesa Huwa Anampa Kiasi hiki.



    Msanii na video queen Gigy Money amesema hawezi kumuweka wazi mpenzi wake kwa sasa, kwani ni mtu ambaye hataki kujulikana na pia anahofia kunyang'anywa na mashoga zakeGigy Money ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, 

    Na kusema kuwa mwandani wake huyo au sponsor kama alivyomuita mwenyewe , ni mtu mzima na msomi, pia ndiye mwanaume pekee ambaye anampa hela nyingi ambazo hakuna mwanaume mwengine anaweza akampatia hapa bongo.

    “Ninae boyfriend... ni sponsor, ambaye alinipenda mimi in and out namuelewa simuelewi najua mimi, ananipa hela nyingi hakuna mwengine, hana kabisa ananipa laki 5, mwenyewe hataki ajulikane, na sitaki kusema naogopa mashoga, mashoga kazi watamgoogle”, alisema Gigy Money.

    Pia Gigy amesema kwamba kitendo cha Rich Mavoko kukataa kuwahi kuwa boyfriend wake huyo hana wivu na maisha yake, lakini pia ni msomi sana.

    “Wivu sijui ameweka pending, nikimtaja wataniogopa,yule mwanaume ana elimu sana, hadi kulala unatumia elimu, kula unatumia elimu, mpaka nimeandikia wimbo unaokuja”, alisema Gigy Money.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Fahamu Kiasi Ambacho Mpenzi wake Gigy kama hana kabisa Pesa Huwa Anampa Kiasi hiki. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top